WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, March 30, 2017

KAMATI YAMHOJI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akipokelewa katika Viwanja vya Bunge na Mkuu wa Kitengo cha Babari, Elimu na Mawasiliano Ndg. Owen Mwandumbya



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda leo amehojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na tuhuma za kuingilia haki, uhuru na madaraka ya Bunge.
Mhe. Makonda aliwasili Bungeni  Dodoma majira ya saa nne asubuhi kuitikia wito wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge  lililotolewa na Bunge, Februari 8, 2017  katika Kikao cha Nane cha Mkutano wa Sita wa Bunge ambapo amehojiwa na kamati hiyo kwa muda wa masaa matatu kuhusu tuhuma zinazomkabili.
Katika kikao hicho, Bunge liliazimia kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti kuitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya Bunge ili kujibu tuhuma hizo.
Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kumaliza kazi yake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George Mkuchika alisema Kamati hiyo imekutana leo baada ya kuagizwa na Mheshimiwa Spika wa Bunge kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.
“Tumefanya kikao hiki cha Kamati baada ya kuagizwa na Mhe. Spika kwa kuwa kwa Mujibu wa Kanuni zetu, Kamati hii inakutana pale tu inapoagizwa na Spika wa Bunge,” alisema.
Alisema Mhe. Spika aliiagiza Kamati hiyo imuite Mhe. Makonda mbele ya Kamati  kufuatia azimio hilo la Bunge lililopitishwa  na Bunge Februari 8, ambapo pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa Mkoa alitakiwa kufika mbele ya Kamati kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Alisema kwa mujibu wa Azimio hilo, Mhe. Makonda alidaiwa kutoa kauli kupitia Televisheni ya Clouds akidai kwamba wabunge wanasinzia Bungeni jambo lililoonekana kwamba ni kudharau Bunge.
“Napenda kutoa taarifa kwamba Mhe. Makonda leo amekuja mbele ya Kamati na ametupa ushirikiano mzuri, tumepokea maelezo yake na Kamati imemaliza kazi yake,” alisema.
Alisema kama ilivyo utaratibu, Kamati yake itakabidhi taarifa yake kwa Mhe. Spika kwa mujibu wa Kanuni ambapo Spika ndiye atakaeamua namna ya kutoa raarifa kuhusu kazi ya Kamati hiyo.
             

Tuesday, March 28, 2017

MAELEZO YA MHE SPIKA WAKATI WA UWASILISHWAJI WA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2017/18


SERIKALI YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2017/18

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa maelezo ya utangulizi kwa Waheshimiwa Wabunge wakati wa Mkutano wa uwasilishaji wa Mpango wa ukomo wa kiwango cha Bajeti uliofanyika leo katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha, 2017/18

Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia Mkutano huo

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongoza Mkutano wa uwasilishaji wa Mpango wa ukomo wa kiwango cha Bajeti uliofanyika leo katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 
 
Na Debora Sanja-Bunge
SERIKALI imewasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha, 2017/18 ambapo imepanga kutumia Sh. Trilioni 31.6.
Taarifa hiyo imewasilishwa Bungeni leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Mkutano wa Wabunge wote kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya Kanuni za Bunge.
Dk. Mpango alisema kati ya kiasi hicho kilichopangwa kutumiwa, fedha zinazotokana na Mapato ya Ndani ni Sh. Trilioni 19. 9 sawa na asilimia 63 huku washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh. Trilioni 3.9 sawa na asilimia 12. 6 na fedha nyingine ni mikopo kutoka soko la ndani.
Aidha, alisema Serikali inatarajia kutumia Sh. Trioni 19.7 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. Trilioni 11. 9 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Akibainisha baadhi ya maeneo ya kipaumbele katika bajeti ya mwaka 2017/18, Dkt. Mpango alisema ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati, kuhuisha Shirika la Ndege Tanzania, ujenzi wa mgodi wa chuma na Kiwanda cha Chuma Liganga Njombe na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma.
“Vipaumbele vingine ni uanzishwaji wa Kanda Maalum ya Kiuchumi Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma na Mtwara, kuendeleza Mradi wa Liquified Natural Gas, kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Makao Makuu Dodoma na kuendeleza Shamba la Kilimo na Uzalishaji Sukari Mkulazi,” alisema.
Kwa upande wake Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aliiagiza Kamati ya Bajeti kuyafanyia kazi mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na Serikali na kuzishauri Kamati za Bunge za Kisekta na Serikali.
“Vilevile mara baada ya kupokea mapendekezo haya, Kamati zote ziandae ratiba ya kuchambua Bajeti za Wizara wanazozisimamia na kazi hii imalizike kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba wa Bunge kwa kuwa haiahirishiki,” alisema.
Aidha, aliwataka Mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wa Serikali kuhakikisha wanashilikiana na Kamati katika uchambuzi wa bajeti za wizara zao.
 

MHE SPIKA ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM



Friday, March 24, 2017

SPIKA WA BUNGE MHE JOB NDUGAI (KUSHOTO) AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC), MHE GUO JINLONG.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akielezea jambo wakati akizungumza na  Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong pamoja na Ujumbe aliombatana nao  Jijini Dare es Salaam. 




Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong akimueleza jambo Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai wakati walipofanya mazungumzo Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifafanua jambo wakati akimkabidhi zawadi Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong mara baada ya kuzungumza nae Jijini Dar es Salaam.



Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kushoto) akifurahia jambo  wakati na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong (katikati) pamoja na Balozi wa China Nchini  Dkt.Lu Youqing (kulia) wakati wakisili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya mazungumzo Jijini Dare es Salaam.