WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 16, 2018

SPIKA AFUNGUA MAFUNZO YA KAMATI YA UONGOZI, MAKAMU WENYEVITI NA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE YANAYOFANYIKA ZANZIBAR

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifurahi kwa pamoja na Maspika wastaafu Mhe. Anna makinda (wa kwanza kushoto) ,Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Kificho, Mhe. Pius Msekwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber A Maulid, wa mwisho ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson. Waheshimiwa Maspika wastaafu wamehudhuria  mafunzo ya Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifungua  mafunzo ya siku  mbili kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiwa Katika picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ambao ni Kamati ya Uongozi ya Bunge, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya utumishi ya Bunge. waliokaa mbele wa kwanza ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber Ali Maulid, Spika Mstaafu Mhe. Anna Makinda, Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa na Katibu wa Bunge Mhe. Stephen kagaigai. Mafunzo hayo yameanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar


Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya siku  mbili kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yaliyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

Wednesday, August 8, 2018

KATIBU WA BUNGE, NDUGU. STEPHEN KAGAIGAI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA




Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Bunge pamoja na maafisa wa ofisi hiyo wanaoshiriki katika Maonyesho ya Naneane yanayoendelea Jijini Dodoma. Katibu alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge kujionea shughuli zinazofanyika katika maonyesho hayo.

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na maafisa wa Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma baada ya kutembelea Banda la Ofisi hiyo. Anayetoa maelezo ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Bi. Zuhura Mtatifikolo.
886

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na maafisa wa Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma baada ya kutembelea Banda la Ofisi hiyo. Anayetoa maelezo ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Bi. Zuhura Mtatifikolo.
886

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akikagua Banda la Ofisi ya Bunge baada ya kutembelea Banda hilo, pembeni ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Bi. Zuhura Mtatifikolo. Ofisi ya Bunge inashiriki katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mwananchi Mkazi wa Jiji la Dodoma ambaye pia ni mlemavu asiyeona akiipapasa SIWA ya mfano baada ya kutembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma

Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akitoa elimu kuhusiana na Bunge kwa wanafunzi  na raia wengine waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma

Monday, August 6, 2018

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DODOMA ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA JIJINI DODOMA

Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuelezea  Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe  orodha ya Maspika waliowahi kuongoza Bunge pamoja na Kumbi zilizowahi kutumika kuendesha vikao vya Bunge.Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuonyesha  Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe kitabu cha viapo vya Waheshimiwa Wabunge cha miaka iliyopita. Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akitoa elimu kwa umma kuhusiana na Bunge kwa wanafunzi wa Shule ya Awali Taqwa wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuonyesha  Mstahiki  Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe vazi la Spika pamoja na kumuelezea historia ya vazi hilo. Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Sunday, August 5, 2018

WANAFUNZI NA WAKAZI WA JIJI LA DODOMA WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE

Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akiwaonyesha kitabu cha majadiliano ya Waheshimiwa Wabunge Bungeni (Hansard) Wanafunzi wa Shule ya Msingi Maria De Mathias wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.



Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akiwalezea wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maria De Mathias namna ya ukaaji wa Waheshimiwa Wabunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.Wanafunzi hao walitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma

Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson Sobha akitoa elimu kuhusiana na Bunge kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Maria De Mathias wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Mohamed Salim akitoa maelezo kuhusu Muundo wa Bunge kwa Bi. Khanifa Hamidu aliyetembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maria De Mathias ya Jijini Dodoma wakifurahia kubeba SIWA ya mfano wakati walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma.
Afisa wa Ofisi ya Bunge  Ndugu Angumbwike Ng’wavi  akiwaonyesha wanafunzi wa Shule ya Msingi Maria De Mathias ya Jijini Dodoma Ukumbi wa Msekwa ambao ulikuwa ukitumiwa kuendeshea vikao vya Bunge kabla ya Ukumbi wa sasa. Wanafunzi hao walitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma

Saturday, August 4, 2018

WAKAZI WA DODOMA WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE


Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda 

akiwaonyesha watoto namna ya ukaaji wa Waheshimiwa 

Wabunge ndani ya Ukumbi wa Bunge, watoto hao walitembelea 

Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea 

Jijini Dodoma


 Watoto waliokuja kutembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma wakifurahia kubeba SIWA ya mfano baada ya kutembelea Banda hilo kwa ajili ya kupata elimu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu Bunge.

Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson Sobha akitoa elimu 

kwa umma kuhusiana na historia ya Bunge kwa wanafunzi 

waliokuja kutembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 

Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Afisa kutoka Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda 

akiwaonyesha wanafunzi kiti ambacho kimewahi kutumiwa na 

Maspika mbalimbali, wanafunzi hao walitembelea Banda la 

Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini 

Dodoma.



Friday, July 27, 2018

WAJUMBE WA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA OFISI YA BUNGE WAKUTANA DODOMA


Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Bunge wakiwa katika kikao leo Mjini Dodoma , kikao hicho kiliongozwa na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai
Wajumbe wakiendelea na Kikao
Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Bunge wakiwa katika kikao leo Mjini Dodoma , kikao hicho kiliongozwa na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai
Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Bunge wakiwa katika kikao leo Mjini Dodoma , kikao hicho kiliongozwa na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai