WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, August 17, 2018

SPIKA WA BUNGE, MHE. JOB NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA MAFUNZO KWA KAMATI YA UONGOZI YANAYOENDELEA KATIKA OFISI NDOGO ZA BUNGE, ZANZIBAR

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge. Kikao hicho kinaendelea kwa siku ya pili katika Ofisi ya Ndogo ya Bunge Zanzibar.anayefuata ni Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Pandu Kificho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai, Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kinachoendelea kwa siku ya pili katika Ofisi ya Ndogo ya Bunge Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kinachoendelea kwa siku ya pili katika Ofisi ya Ndogo ya Bunge Zanzibar.

Wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge wakimsikiliza mtoa mada kutoka Idara ya Usalama, Ndugu Mluli Mahendeka katika semina ya kuwajengea uwezo inayofanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Zanzibar. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza kikao cha mafunzo cha mafunzo hayo.


TAARIFA KUHUSU KUANZA KWA SHUGHULI ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE JIJINI DODOMA KUANZIA TAREHE 20 AGOSTI HADI 2 SEPTEMBA, 2018.



SPIKA WA BUNGE, MHE. JOB NDUGAI PAMOJA NA UJUMBE WAKE WAMTEMBELEA RAIS WA ZANZIBAR MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEI

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai. Mheshimiwa Ndugai pamoja na ujumbe wake  ambao ni wawakilishi wa Kamati ya Bunge ya Uongozi na wawakilishi wa Tume ya Utumishi ya Bunge walikwenda kumtembelea Mhe. Shein leo Ikulu Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai. Mheshimiwa Ndugai pamoja na ujumbe wake  ambao ni wawakilishi wa Kamati ya Bunge ya Uongozi na wawakilishi wa Tume ya Utumishi ya Bunge walikwenda kumtembelea Mhe. Shein leo Ikulu Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Oscar Mukasa, Mhe. Mary Chatanda, Mhe.Fakharia Shomar Khamis, Mhe. Mussa Azzan Zungu na Mhe. Freeman Mbowe.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein .Mheshimiwa Ndugai pamoja na ujumbe wake  ambao ni wawakilishi wa Kamati ya Bunge ya Uongozi na wawakilishi wa Tume ya Utumishi ya Bunge walikwenda kumtembelea Mhe. Shein leo Ikulu Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  pamoja na ujumbe wake  ambao ni wawakilishi wa Kamati ya Bunge ya Uongozi na wawakilishi wa Tume ya Utumishi ya Bunge walikwenda kumtembelea Mhe. Shein leo Ikulu Zanzibar.