WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, May 21, 2021

WATUMISHI OFISI YA BUNGE WAMPOKEA KATIBU MPYA WA BUNGE JIJINI DODOMA


Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi akipokelewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Bunge, Ndg. Triphonia Mng’ong’o alipowasili katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.


Watumishi Ofisi ya Bunge wakimpokea kwa bashasha Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi alipowasili katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi (Mwenye maua) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Bunge nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Katibu wa Bunge, Ndg, Nenelwa Mwihambi (katikati mbele) katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Bunge nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wanne kushoto mbele ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama




 

BUNGENI 21.05.2021


 

Wednesday, May 19, 2021

KATIBU MPYA WA BUNGE, BI. NENELWA MWIHAMBI AAPISHWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi akiapa kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma baada ya kuapishwa kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi.  Nenelwa Mwihambi akiapa Ikulu Jijini Dar es Salaam

 

Saturday, May 15, 2021

MHE. RAIS SAMIA AMTEUA BI. NENELWA MWIHAMBI KUWA KATIBU WA BUNGE

 

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua  Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano  Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Bi. Mwihambi anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa Bunge Bi. Mwihambi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge.

Aidha, Bi. Mwihambi anakuwa Mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge.

Friday, May 14, 2021