WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, October 19, 2023

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU WAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA UJENZI KUHUSU UTENDAJI WA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA).















Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso wamepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Ujenzi kuhusu utendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha Julai - Oktoba, 2023; Mafanikio na Changamoto katika kikao kilichofanyika leo tarehe 19 Oktoba, 2023 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro.



 

Tuesday, October 3, 2023

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE




 


TIMU ZA BUNGE ZAENDELEA KUFANYA VIZURI KATIKA MICHEZO YA SHIMIWI MKOANI IRINGA





Timu za Klabu ya michezo za Bunge zimeendelea kufanya vizuri katika michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea leo tarehe 3 Oktoba Mkoani Iringa.

Timu ya kamba wanawake imeigaragaza timu ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa pointi 2-0 huku timu ya kamba wanaume ikiiburuza timu ya Ujenzi kwa pointi 1-0 wakati wa mchezo uliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.

Nayo timu ya netiboli imeibuka kidedea baada ya kuibugiza magoli 31 - 16 timu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati wa mchezo uliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU).

Kwa upande wa timu ya soka ya Bunge imeicharaza goli 2 -1 timu ya soka ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM Samora Mkoani hapa.

Michezo SHIMIWI inaendelea kutimua vumbi Katika viwanja mbalimbali na inategemewa kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba, 2023, Mkoani Iringa.

Saturday, September 2, 2023

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI WAKATI WA NMB BUNGE BONANZA









Matukio katika picha yaliyojiri wakati wa NMB Bunge Bonanza  katika michezo ya Mpira wa Wavu, Kurusha Tufe, Karata, Draft na Pool Table leo tarehe 2 Septemba, 2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin, Jijini Dodoma.

Katika michezo hiyo, mgeni rasmi alikuwa ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid.