Katibu wa Bunge
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc amehairisha kikao cha Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge baada
ya kusoma na kuridhia maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.
Kikao hicho
kimehairishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023 katika hoteli na kituo cha Mikutano
cha APC kilichopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Maazimio mbalimbali
yalifikiwa katika kikao hicho ikiwemo kuendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango
kazi wa ofisi ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mwaka wa fedha
2023/2024 yanatimia na baada ya mpango wa maendeleo wa Taifa kupitishwa na
Bunge idara na vitengo vianze mchakato wa kuweka vipaumbele katika kutenga
Bajeti hususan kwa miradi ya inayoendelea. Aidha, kwa miradi mipya maandiko ya
miradi ikamilike na yapitishwe katika hatua zote muhimu za maamuzi kabla ya
kutenga Bajeti.
Akizungumza wakati
wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali
na Sekta ya Afya (TUGHE)Taifa ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu TUGHE Taifa, Ndg.
Brendon Maro amempongeza Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa ushindi
alioupata wa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
“Ushindi wake
umekuja kwa kuwa ana mtandao mmoja kutoka kwenye taasisi yake anayoifanyia kazi
hasa watumishi wamesaidia sana”amesema Maro
Awali, akizungumza
wakati akihairisha kikao hicho Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc
ameshukuru kwa salamu hizo zilizotolewa na TUGHE Taifa kwa Mhe. Spika na
kuhaidi kumfikishia, Pia alihimiza watumishi wafanye kazi kwa bidii ili ilete
tija kwa Bunge na Taifa.
Kikao hicho cha
muda wa siku mbili kimeanza jana tarehe 17 Novemba, 2023 na kimehitimishwa leo
tarehe 18 Novemba, 2023.