WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, January 9, 2024

VIONGOZI WA DINI, VYAMA VYA SIASA WAMEENDELEA KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MINNE YA SHERIA ILIYOSOMWA BUNGENI KWA MARA YA KWANZA


Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Florent Kyombo na Katibu wa kamati hiyo, Ndg. Frank Nkya.


Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo akitoa maoni wakati wa uotaji wa maoni ya wadau mbalimbali kuhusu Miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2024 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni, Jijini Dodoma.




Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe. Mary Chatanda akitoa maoni kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uotaji wa maoni ya wadau mbalimbali kuhusu Miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2024 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni, Jijini Dodoma.



Mbunge Mstaafu na Mwakilishi kutoka NCCR Mageuzi, Mhe. Joseph Selasini akitoa maoni kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Khadija Taya akichangia jambo wakati wa utoaji wa maoni kwa wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Wadau Mbalimbali wakifuatilia utoaji wa maoni kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 9 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.


Saturday, January 6, 2024

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA YAPOKEA MAONI YA WADAU MBALIMBALI

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 6 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Florent Kyombo na Katibu wa kamati hiyo, Ndg. Frank Nkya.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya  Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023]. 


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale, Mhe. Hussein Nassor Amar akichangia jambo wakati wa utoaji wa maoni kwa wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 6 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya  Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023]. 


Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe akitoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; wakati wa utoaji wa maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 6 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia maoni ya wadau kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 6 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya  Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023]. 



Wadau Mbalimbali wakifuatilia utoaji wa maoni kuhusu miswada minne ya Sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge leo tarehe 6 Januari, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya  Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023].

KAMATI YA BUNGE YA PIC YASHIRIKI SEMINA YA MSAJILI WA HAZINA 5-6 JANUARI 2024








 

Thursday, January 4, 2024

SPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA 27 LA MASPIKA NA WENYEVITI WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA






Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 27 la Maspika na Wenyeviti wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola uliofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024, Kampala nchini Uganda.

Kongamano hilo limefunguliwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni.

Kongamano hilo pamoja na mambo mengine linatoa fursa kwa Maspika kubadilishana uzoefu wa  uendeshaji bora wa Mabunge. Katika Kongamano hilo linaloendelea hadi tarehe 6 Januari 2024, mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja ya kibunge.


 

Friday, December 8, 2023

WACHEZAJI WA TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB WASHIRIKI UFUNGUZI WA MICHEZO YA 13 YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KIGALI NCHINI RWANDA.











Wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Tarimba Abbas wameshiriki katika ufunguzi wa michezo ya 13 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofanyika Kigali nchini Rwanda.

Mashindano hayo yamefunguliwa leo tarehe 8 Disemba, 2023 na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Donatile Mukabalisa.

Huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni kwa maendeleo, amani na Jumuiya yote ya Afrika Mashariki.


 

Saturday, November 18, 2023

KATIBU NENELWA AHAIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE, TUGHE TAIFA YAMPONGEZA SPIKA DKT. TULIA KWA USHINDI WA URAIS WA IPU
















Katibu wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc amehairisha kikao cha Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge baada ya kusoma na kuridhia maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Kikao hicho kimehairishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023 katika hoteli na kituo cha Mikutano cha APC kilichopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Maazimio mbalimbali yalifikiwa katika kikao hicho ikiwemo kuendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango kazi wa ofisi ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 yanatimia na baada ya mpango wa maendeleo wa Taifa kupitishwa na Bunge idara na vitengo vianze mchakato wa kuweka vipaumbele katika kutenga Bajeti hususan kwa miradi ya inayoendelea. Aidha, kwa miradi mipya maandiko ya miradi ikamilike na yapitishwe katika hatua zote muhimu za maamuzi kabla ya kutenga Bajeti.

Akizungumza wakati wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya Afya (TUGHE)Taifa ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu TUGHE Taifa, Ndg. Brendon Maro amempongeza Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa ushindi alioupata wa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

“Ushindi wake umekuja kwa kuwa ana mtandao mmoja kutoka kwenye taasisi yake anayoifanyia kazi hasa watumishi wamesaidia sana”amesema Maro

Awali, akizungumza wakati akihairisha kikao hicho Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc ameshukuru kwa salamu hizo zilizotolewa na TUGHE Taifa kwa Mhe. Spika na kuhaidi kumfikishia, Pia alihimiza watumishi wafanye kazi kwa bidii ili ilete tija kwa Bunge na Taifa.

Kikao hicho cha muda wa siku mbili kimeanza jana tarehe 17 Novemba, 2023 na kimehitimishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023.