WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Sunday, December 8, 2024

TIMU NNE ZA BUNGE LA TANZANIA LEO ZIMECHUANA NA TIMU MBALIMBALI KATIKA MASHINDANO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA MOMBASA KENYA

 

Mfungaji wa bao la pekee wa mchezo katika ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki akichauna vikali na mpinzani wake wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Mpira wa Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanaume wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya.

Mchezaji wa Mpira wa pete kutoka Timu ya Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Esther Matiko akijiandaa kufunga wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) katika mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya na ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga EALA mabao 50-0

Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Bunge ya Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

 

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana kabla ya kuanza kwa mchezo na Timu ya Bunge la EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana akisalimiana na Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Pete kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata wakati timu hiyo ikijiaanda kuingia uwanjani kuchuana na Timu ya EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.

Saturday, December 7, 2024

PICHA ZA UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, MOMBASA KENYA

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Likoni kwa ajili ya hafla ya ufunguzi wa wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Abbas Tarimba akizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024.



 Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya 6-17 Desemba, 2024 huku Timu ya Bunge ikiwa inashiriki michezpo mbalimbali

Waheshimiwa Wabunge ambao ni wanamichezo wa timu mbalimbali za Bunge wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024
 

Wednesday, November 13, 2024

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson amekabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Maspika kwa Spika wa Kenya katika Mkutano uliofanyika Nairobi, Kenya

 

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Nairobi Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Tulia alikabidhi nafasi ya Mwenyekiti kwa Spika wa Bunge la Kenya Moses Wetang’ula
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akipeana mkono  na Spika wa Bunge la Kenya Mheshimiwa Moses Wetang’ula mara baada ya kumkabidhi nafasi ya Mwenyekiti  wa Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Tulia ameshika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Maspika wa EAC uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya

Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Uganda Mheshimiwa Anita Among na Spika wa Bunge la Mpito la Sudan ya Kusini Mheshimiwa Jemma Kumba wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maspika wa Bunge na Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa Nchi hizo uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya
Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maspika wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipohudhuria Mkutano wa Maspika wa nchi hizo uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya

Monday, November 11, 2024

Katibu wa Bunge amekabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Katibu wa Bunge la Kenya

Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akishikana mkono na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi Kenya.
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akiwa pamoja na Naibu Katibu wa Bunge la Kenya Ndugu Jeremiah Ndombi mara baada ya kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Bunge la Kenya. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa Makatibu unaofanyika Nairobi Kenya
Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard akizungumza katika Mkutano wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano  huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya

Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndugu Baraka Leonard (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada kukabidhi nafasi ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya kwa Bunge la Kenya. Mkutano  huo wa Makatibu unafanyika Jijini Nairobi Nchini Kenya.

 

Wednesday, November 6, 2024

NAIBU SPIKA ZUNGU AONGOZA MAZUNGUMZO KUHUSU MASUALA YA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDG’S)
















Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza mazungumzo kati ya Wabunge wa Bunge la Tanzania wa Mtandao kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’S) na Wabunge wa Bunge la Kidemokrasia ya Congo wa Mtandao kuhusu masuala ya SDG’S.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 6 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Spika, Bungeni Jijini Dodoma.

Dhumuni la mazungumzo hayo ni kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo kuondoa umaskini, kuleta usawa na kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mmoja.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Zungu alisisitiza,  Wabunge kuendelee kuunga mkono juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala ya malengo ya Maendeleo endelevu. 

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania Nchini Congo, Mhe. Said Mshana.