WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, November 22, 2018

SPIKA WA BUNGE LA VIJANA AONGOZA KIKAO CHA PILI CHA BUNGE LEO JIJINI DODOMA

Katibu wa Bunge la Vijana Ndugu Alhoncina S. Ambrosi (mwenye koti la bluu katikati) akiwapa utaratibu waheshimiwa wabunge kabla ya kuanza kikao cha pili cha Bunge la Vijana.
Spika wa Bunge la Vijana Mheshimiwa Zephania Sane aogoza kikao cha pili cha Bunge la Vijana kilichofanyika katika ukumbi wa Msekwa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma.
Bunge la Vijana laendelea leo jijini Dodoma. kikao hicho kilianza mapema saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa Msekwa uliopo katika viwanja vya Bunge.

Wednesday, November 21, 2018

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE OFISINI KWAKE LEO

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifurahi jambo na mgeni wake Mheshimiwa balozi wa Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen alipomtembelea ofisini kwake mapema leo hii. 
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na mgeni wake Mheshimiwa balozi wa Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen alipomtembelea ofisini kwake mapema leo hii.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na mgeni wake Mheshimiwa balozi wa Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen alipomtembelea ofisini kwake mapema leo hii. Spika alimtaarifu balozi kuwa alishawahi kusoma nchini Norway.
Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania Mheshimiwa Elisabeth Jacobsen amemtembelea Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ofisini kwake Bungeni mapema leo hii. Balozi amempa salamu nyingi Mheshimiwa Spika kutoka Serikali anayoiwakilisha.

SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI AFUNGUA MKUTANO WA BUNGE LA VIJANA JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiapa kushika nafasi hiyo mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Ndugu Alphonsina Ambrosi. Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018 unaendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Mapambe  wa Bunge akiongoza msafara wa Spika wa Bunge la Vijana kuingia Ukumbini kwa ajili ya kuanza Kikao cha Kwanza cha Bunge hilo kwa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana  mwaka 2018 wa wakila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge hilo la vijana, Mhe. Zaphania Sane.wengine ni Makatibu Kamati wa Bunge hilo.
Spika wa Bunge wa Bunge , Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana mwaka 2018 Mhe. Zephania Sane kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge hilo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Mhe. Ndugai alikuwa mgeni ramsi na alifungua  Bunge hilo la Vijana
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Bunge la Vijana  mwaka 2018 linalofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma kulia kwake ni Spika wa Bunge la Vijana Mhe. Zephania Sane na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Ashiruna Mhunzi
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Bunge la Vijana  mwaka 2018 linalofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma kulia kwake ni Spika wa Bunge la Vijana Mhe. Zephania Sane na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Ashiruna Mhunzi
Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018 unaoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Friday, November 16, 2018

MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA CHINA ATEMBELEA BUNGE LA TANZANIA JIJINI DODOMA




Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto). Makamu huyo wa Rais akiambatana na Wabunge kumi na tano wametembelea Bunge la Tanzania kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng pamoja na Ujumbe wake walipotembelea Bunge mapema leo. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, Balozi China nchini Bi. WANG Ke na baadhi ya Wabunge kutoka Bunge la Tanzania na Wabunge kumi na tano kutoka Bunge la China.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto) mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.




Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng (kushoto) mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng, (wa pili kutoka kushoto) Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (wa pili kutoka kulia) Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa kwanza kulia) na Balozi China nchini Bi. WANG Ke (wa kwanza kushoto) mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Mhe. CAI Dafeng mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi China nchini Bi. WANG Ke.