WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, April 21, 2023

SPIKA DKT. TULIA, KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE WAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI TEULE YA MHE. RAIS YA KUTATHMINI UFANISI NA UTENDAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya (Kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mstaafu Hassan Yahya akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya Wajumbe wa kamati hiyo na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (hayupo kwenye picha) kilichofanyika leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.




Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika kikao na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (hayupo kwenye picha) walipomtembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akiongoza kikao kati ya Wajumbe wa Kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya (kushoto kwake) walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Cosato Chumi akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika kikao cha kamati hiyo na Wajumbe wa Kamati teule ya Mhe. Rais ya kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwenyekiti, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Yahya walipowatembelea leo tarehe 20 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Neema Lugangira, Mbunge wa Lupembe, Mhe. Edwin Swalle na Mbunge wa Ukerewe, Mhe. Joseph Mkundi.

Tuesday, February 28, 2023

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAFUNZO YA KAMATI YA UONGOZI NA MAKAMU WENYEVITI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE TUNGUU, ZANZIBAR


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kabla ya kufungua mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar



Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifungua mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar, Kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge uliofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar, Kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi.




Wajumbe wa Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu wakishiriki katika ufunguzi wa mafunzo ya kamati hizo zilizofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar




Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge mara baada ya kufungua mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar, Waliokaa Kulia kwake ni Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc (kulia), Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Riziki Lulida (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi



Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Bunge mara baada ya kufungua mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar, Waliokaa Kulia kwake ni Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc (kulia), Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Riziki Lulida (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi



Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kabla ya kufungua mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 28 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar


 

Monday, February 27, 2023

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA MAFUNZO YA KAMATI YA UONGOZI NA MAKAMU WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uongozi, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza mafunzo ya kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akitoa neno la ukaribisho kwa Wajumbe wakati wa mafunzo ya Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar, Katikati ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uongozi, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda



Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akitoa neno la utangulizi wakati wa mafunzo ya Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar



Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda akitoa mada kuhusu Madaraka, Majukumu, Mipaka ya Utendaji Kazi, Uzoefu na Changamoto katika Uendeshaji wa Kamati za Bunge wakati wa  mafunzo ya Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar



Mkufunzi wa Mafunzo Kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute), Ndg. Zuhura Muro akitoa mada kuhusu Uongozi wa Kimkakati katika uendeshaji wa Shughuli za Bunge wakati wa mafunzo ya Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar






Wajumbe wa Kamati ya uongozi na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge wakiwa katika mafunzo kuhusu Madaraka, Majukumu, Mipaka ya Utendaji Kazi, Uzoefu na Changamoto katika Uendeshaji wa Kamati za Bunge na Uongozi wa Kimkakati katika uendeshaji wa Shughuli za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 27 Februari, 2023 katika ofisi ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar