WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, January 4, 2024

SPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA 27 LA MASPIKA NA WENYEVITI WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA






Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 27 la Maspika na Wenyeviti wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola uliofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024, Kampala nchini Uganda.

Kongamano hilo limefunguliwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni.

Kongamano hilo pamoja na mambo mengine linatoa fursa kwa Maspika kubadilishana uzoefu wa  uendeshaji bora wa Mabunge. Katika Kongamano hilo linaloendelea hadi tarehe 6 Januari 2024, mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja ya kibunge.


 

Friday, December 8, 2023

WACHEZAJI WA TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB WASHIRIKI UFUNGUZI WA MICHEZO YA 13 YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KIGALI NCHINI RWANDA.











Wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Tarimba Abbas wameshiriki katika ufunguzi wa michezo ya 13 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayofanyika Kigali nchini Rwanda.

Mashindano hayo yamefunguliwa leo tarehe 8 Disemba, 2023 na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Donatile Mukabalisa.

Huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni kwa maendeleo, amani na Jumuiya yote ya Afrika Mashariki.


 

Saturday, November 18, 2023

KATIBU NENELWA AHAIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE, TUGHE TAIFA YAMPONGEZA SPIKA DKT. TULIA KWA USHINDI WA URAIS WA IPU
















Katibu wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc amehairisha kikao cha Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge baada ya kusoma na kuridhia maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Kikao hicho kimehairishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023 katika hoteli na kituo cha Mikutano cha APC kilichopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Maazimio mbalimbali yalifikiwa katika kikao hicho ikiwemo kuendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango kazi wa ofisi ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 yanatimia na baada ya mpango wa maendeleo wa Taifa kupitishwa na Bunge idara na vitengo vianze mchakato wa kuweka vipaumbele katika kutenga Bajeti hususan kwa miradi ya inayoendelea. Aidha, kwa miradi mipya maandiko ya miradi ikamilike na yapitishwe katika hatua zote muhimu za maamuzi kabla ya kutenga Bajeti.

Akizungumza wakati wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya Afya (TUGHE)Taifa ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu TUGHE Taifa, Ndg. Brendon Maro amempongeza Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa ushindi alioupata wa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

“Ushindi wake umekuja kwa kuwa ana mtandao mmoja kutoka kwenye taasisi yake anayoifanyia kazi hasa watumishi wamesaidia sana”amesema Maro

Awali, akizungumza wakati akihairisha kikao hicho Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc ameshukuru kwa salamu hizo zilizotolewa na TUGHE Taifa kwa Mhe. Spika na kuhaidi kumfikishia, Pia alihimiza watumishi wafanye kazi kwa bidii ili ilete tija kwa Bunge na Taifa.

Kikao hicho cha muda wa siku mbili kimeanza jana tarehe 17 Novemba, 2023 na kimehitimishwa leo tarehe 18 Novemba, 2023.

 

Friday, November 17, 2023

KATIBU NENELWA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE JIJINI DAR ES SALAAM


















Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc ameongoza kikao cha Baraza hilo kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya idara ya utawala na rasilimali watu kwa Mwezi Julai - Septemba 2023 kilichofanyika katika hoteli na Kituo cha Mikutano cha APC Jijini Dar es Salaam.