Monday, May 6, 2024
Monday, April 15, 2024
SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI BUNGE MARATHON
SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI BUNGE MARATHON
·
Ashiriki katika mbio za km 5
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), mgeni rasmi katika
mbio za Bunge Marathon zilizofanyika tarehe 13 Aprili, 2024 katika Uwanja wa
Jamhuri Jijini Dodoma.
Mbio hizo za Bunge marathon zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Katibu Tawala Mkoa wa
Dodoma, Ndg. Kaspar Mmuya, Waheshimiwa Wabunge na Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc.
Lengo likiwa ni kuchangisha kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa ajili
ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Bunge.
Huku kauli mbiu ikiwa ni “Shiriki Michezo kwa Maendeleo ya Taifa
Letu”.
Tuesday, March 26, 2024
KAMATI YA LAAC IMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA MKAONI SIMIYU KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA JENGO LA DHARULA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA HIYO NA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA CHAKI
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia vifaa vya matibabu katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Moan Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakionyeshwa mojawapo ya mtambo wa kutengeneza chaki wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami kilichopo Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akizungumza na watendaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.Sunday, March 24, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MRADI WA SHULE YA SEKONDARI NA ZAHANATI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata ya Kigera katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalus Mabula akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na mradi wa ujenzi wa Zahati ya Rwamlimi katika Manispaa hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stanslaus Mabula akizungumza wakati Kamati ya LAAC ilipomtembelea Mkuu wa Mkoa Ofisini kwake katika Manispaa ya Musoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mtanda na kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mheshimiwa Patrick Gumbo.Saturday, March 23, 2024
KAMATI YA BUNGE YA LAAC IMETEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua ujenzi wa msingi katika moja ya wodi ya Hospitali ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Marawakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo.Friday, March 22, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MRADI WA SOKO NA JENGO LA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalus Mabula akizungumza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Soko hilo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula wakionyeshwa mchoro wa ramani ya Soko Kuu la Kisasa lililopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Soko hilo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula wakikagua mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa lililopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.Thursday, March 21, 2024
WAJUMBE WA KAMATI YA LAAC WAMETEMBELEAA NA KUKAGUA MIRADI MIWILI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiangalia mchoro wa ramani ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula pomoja na Mjumbe wa Kamati Mheshimiwa Suma Fyandomo wakiangalia ujenzi wa maabara ya kemia kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo Kijiji cha Nyasaricho katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua mradi wa la Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo.




















