Friday, January 31, 2025
Tuesday, January 28, 2025
Monday, January 27, 2025
Wednesday, January 15, 2025
WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE WAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA CPA NA JUKWAA LA MAZIWA MAKUU

Monday, December 9, 2024
TIMU ZA TANZANIA ZANG'ARA MASHINDANO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA MOMBASA NCHINI KENYA
Wachezaji za Bunge la Tanzania wakishangilia ushindi walioupata katika michezo mbalimbali katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanaume wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo.
Wachezaji za Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mheshimiwa Salma Kikwete wakishangilia ushindi wa riadha katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanawake wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo

Mchezaji wa Timu ya Riadha kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Anatropia Theonist akishiriki katika mbio za mita 1500 katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya. Mheshimiwa Anatropia alishika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na mbio za mita 400

Timu ya Bunge ya Mpira wa Wavu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo kati yao na Timu ya Bunge ya Sudan ya Kusini kushindwa kufanyika kutokana na timu hiyo kutofika uwanjani. Timu za Bunge la Tanzania zipo Mombasa Nchini Kenya kushiriki michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Sunday, December 8, 2024
TIMU NNE ZA BUNGE LA TANZANIA LEO ZIMECHUANA NA TIMU MBALIMBALI KATIKA MASHINDANO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA MOMBASA KENYA
Mfungaji wa bao la pekee wa mchezo katika ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki akichauna vikali na mpinzani wake wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Mpira wa Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya.

Mchezaji wa Mpira wa pete kutoka Timu ya Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Esther Matiko akijiandaa kufunga wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) katika mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya na ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga EALA mabao 50-0
Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Bunge ya Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana kabla ya kuanza kwa mchezo na Timu ya Bunge la EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana akisalimiana na Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Pete kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata wakati timu hiyo ikijiaanda kuingia uwanjani kuchuana na Timu ya EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.
Saturday, December 7, 2024
PICHA ZA UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, MOMBASA KENYA

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Abbas Tarimba akizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024.























