WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 7, 2016

SPIKA AFUNGUA MKUTANO KATI YA BAADHI YA WABUNGE NA WADAU WA AFYA.

Spika wa  Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mtaalamu  Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson. Walikuwa wakizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano uliowahusisha baadhi ya Wabunge na wadau wa Afya. Mkutano huo ulilenga kujadili kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Afya na ulifayika leo tarehe 3 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano wa pamoja na wadau wa Afya kujadaili kuhusu uwekezaji katika sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano wa pamoja na wadau wa Afya kujadaili kuhusu uwekezaji katika sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kushoto), Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala  pamoja na Mtaalamu  Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya. Anayezungumza ni Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora.

Baadhi ya Wabunge  na Wadau wa Afya wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya hapa nchini.

Spika wa  Bunge Mhe Job Ndugai akihutubia wadau mbalimbali wa Afya waliokutana kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa nchini.

Spika wa  Bunge Mhe Job Ndugai (kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora  (katikakati) na na Mtaalamu  Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakijadili jambo mara baada ya ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hpa nchini.

No comments:

Post a Comment