WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, May 13, 2016

MATUKIO YA UWASILISHWAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, BUNGENI DODOMA.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Zamaradi Kawawa wakiwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajli ya kusikiliza Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 13 Mei, 2016.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma leo 13 Mei, 2016.

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (katikati), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (kushoto) pamoja na mgeni mwingine aliyealikwa wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo wakifuatilia Bajeti ya Wizara hiyo ikiyowasilishwa na Waziri Nape Nnauye Bungeni hapo mjini Dodoma 13 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) ndani ya Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) wakijadiliana jambo ndani ya Bunge mjini Dodoma.

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (katikati), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Zawadi Msalla (kushoto) pamoja na Katibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bi, Anna Nkinda wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo leo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Kundi la Wasanii na Bloggers Bungeni mjini Dodoma 13 Mei, 2016.(Picha/Benedict Liwenga,Dodoma)

No comments:

Post a Comment