WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, June 7, 2016

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO WA PILI WA MAENDELEO

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kwa ajili ya uzindua wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzindua wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiimba wimbo kabla ya kuzindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma. Pamoja naye (kutoka kushoto) ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Mawaziri pamoja na Wabunge mbalimbali  wakiimba wimbo kabla ya uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma leo. Pamoja naye (kutoka kushoto) ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akipokea Kitabu cha Mpango  kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Mpango huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akionesha  Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano  alichopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Mpango huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Mawaziri, Wabunge pamoja Viongozi mbalimbali  wakiimba wimbo kabla ya uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma

No comments:

Post a Comment