KAMATI YA LAAC YAFANYA MAHOJIANO NA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Seif Gulamali
akichangia katika Kikao cha Kamati hiyo leo Mjini Dodoma. Kamati ilikuwa
ikiihoji Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhusu hesabu za mwaka wa fedha 2014/15.
Mweka Hazina wa Halmshauri ya Jiji la Arusha,
Ponceano Kilumbi akijibu hoja za wabunge katika kikao cha Kamati ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC) Mjini Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa Jiji hilo,
Athumani Kihamia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC), (mwenye shati jeupe) Mheshimiwa
Vedasto Ngombale akizungumza jambo katika kikao cha Kamati hiyo leo Mjini
Dodoma.Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Abdalla Chikota.
No comments:
Post a Comment