WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, November 16, 2016

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUTOKA NCHI ZA NORDIC      Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo mbele ya Wadau wa Maendeleo kutoka Timu ya Ujumbe kutoka Nchi za Nordic uliomtembelea Ofisini kwake Dodoma leo kujionea utekelezaji wa Mradi wa Legislature Support Project II unaotekelezwa na Bunge kwa ufadhili  wa wadau hao kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Ujumbe huo uliongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro Rodriguez (Kulia kwake) na Bi. kit Clausen Mshauri Mwandamizi wa Ubalozi wa Denmark katika Umoja wa Mataifa Mjini New York - Marekani.


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Bi. kit Clausen, Mshauri Mwandamizi wa Ubalozi wa Denmark katika Umoja wa Mataifa Mjini New York - Marekani wakati akifafanua jambo wakati wadau hao kutoka Nchi za Nordic walipomtembelea Ofisini kwake Dodoma leo.

Wadau wa Maendeleo kutoka Timu ya Ujumbe kutoka Nchi za Nordic walipomtembelea Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ofisni kwake leo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment