Wabunge wafundwa kuhusu Mktaba wa EPA
Wabunge
wamepewa Semina kuhusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya (EPA).
Semina
hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma ambapo watoa mada walikuwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda , Bishara na
Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda akishirikiana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao
ni Prof. Palamagamba Kabudi, Dkt.
Ng’wanza Kamata na Dkt. John Njigu.
Wakizungumza
katika nyakati tofauti Wasomi hao waliwaasa Waheshimiwa Wabunge kuusoma mkataba
huo kwa kina ili waweze kufanya mamuzi
sahihi huku wakikumbusha kuwa hatima ya Mkataba huo ipo mikononi mwa Waheshimiwa
Wabunge ambao ndiyo wanaoweza kuukubali au kuukataa mkataba.
Mkataba
huo unatarajiwa kujadiliwa kwa kina Bungeni katika Mkutano huu wa Bunge Novemba
10, mwaka huu ambapo Wabunge watapata fursa ya ya kujadili na kuishauri
Serikali kuhusu kuukubali au kuukata Maktaba huo.
Awali
kabla ya kuanza kwa semina hiyo, Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai alisema
semina hiyo ni muhimu katika kuwasaidia Waheshimiwa Wabunge kuweza kufanya maamuzi sahihi juu ya Mkataba
huo.
“Semina
hii ni muhimu kwetu wabunge ili kuweza kupata uelewa kuhusiana na Maktaba huu
wa EPA ili siku tutakayokuja kujadili tutoe ushauri mzuri kwa Serikali kwa
manufaa ya Taifa letu,” alisema Mhe Spika.
Wakichangia
katika nyakati tofauti Waheshmiwa Wabunge walisema elimu waliyoipata kuhusu
Mkataba huo imekuja wakati mwafaka wakati wanatarajia kuujadili, na hivyo
katika siku zilizosalia watausoma kwa kina Mkataba huo kabla ya kuja kuujadili Bungeni
kuhusu kuupitisha au kutopitisha Mkataba huo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.
Dalaly Kafumu alisema anashukuru kwamba Waheshimiwa Wabunge
wamepata Semina kuhusu Mkataba huo na hivyo akawasisitiza kwenda kusoma
mktaba
huo ili waweza kuwa na uelewa mpana kabla ya kuja kuujadili Bungeni
Pamoja na
Waheshimiwa Wabunge na Mawaziri, Semina hiyo kuhusu Mktaba wa EPA ilihudhuriwa pia
na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim
Majaliwa na Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson.
No comments:
Post a Comment