WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, January 19, 2017

KAMATI YA ARDHI, MALISILI NA UTALII YATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwasili katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam, wa kwanza mbele ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Ramo Makani, Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Atashista Nditiye na Mbunge wa Lushoto Mheshimiwa Mheshimiwa Shaban Shekilindi.

Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia burudani ya ngoma za asili wakati walipotembelea Kijiji cha Makumbusho.

Mtaalamu kutoka Kijiji cha Makumbusho, Ndugu Mawazo Ramadhani akitoa maelezo kuhusiana na nyumba ya jamii ya wachaga kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Achiles Bufwe akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Hati ya Uhuru iiyosainiwa na Malkia Elizabeth na Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wajumbe hao walipotembelea Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kuona fuvu la binadamu wa kwanza (Zinjathropas).

No comments:

Post a Comment