Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job akipokea zawadi kutoka
Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai
yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko wa Spika wa Bunge
la Kenya Mhe Justin Muturi ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya
Utumishi ya Bunge,Mhe Mary Chatanda,Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter
Msigwa.
Aidha akizungumza alipokutana na Spika Wa Bunge la Kenya
Mhe Ndugai amesema kuwa alipokea mwaliko wa kutembelea Bunge la Kenya
kutoka na historia kubwa ambayo mabunge yote mawili yanao.
"Mabunge yetu mawili yamekuwa na ushirikiano mkubwa kwa miaka mingi," alisema Mhe Ndugai.
Kwa upande wake Spika Wa Bunge la Kenya Mhe Muturi alisema "tumefurahi
kwa kukubali mwaliko wetu na kuambatana na wabunge.Kupitia ziara yako
nina imani sote wawili tutajifunza mengi katika uendeshaji Bunge hususan
kwa mabadiliko ambayo hapa Kenya tumefanya".
|
No comments:
Post a Comment