MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA UGANDA WAKUTANA NA MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA TANZANIA
Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Kamishina
wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao baina ya Makamishina wa Tume
ya Utumishi wa Bunge la Uganda na
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za
Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao baina ya Makamishina hao ambacho lengo kubwa
lilikuwa ni kubadilishana uzoefu wa utedaji kazi kiliongozwa na Mhe Zungu kwa niaba ya Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ambaye
ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania. Makamishina hao wa
Bunge la Uganda wapo nchini kwa ziara ya Kibunge ya siku mbili.
Kikao kikiendelea
Kiongozi wa Msafara Makamishina wa
Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe CeciliaOgwal (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya Makamishina
wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za
Bunge Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge mbaye pia ni Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akizungumza
wakati wakikao baina ya Makamishina wa
Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge
Jijini Dar es Salaam.
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la
Uganda na Makamishina wa Tume ya
Utumishi wa Bunge la Tanzania (waliokaa)
na baadhi ya Watumishi wa pande zote mbili katikapicha ya pamoja mara baada ya kikao.
No comments:
Post a Comment