WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, October 31, 2017

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali 

za Mitaa wakiwa katika kikao na Watendaji wa Ofisi 

ya 

Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala 

ambapo walijadili  Taarifa ya Maboresho ya 

Mfumo wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS), 

Kulia kwake ni Katibu wa Kamati hiyo, Eunike Shirima.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi 

wa Umma na Utawala, Mheshimiwa George 

Mkuchika  akisoma Taarifa ya Maboresho ya Mfumo 

wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS) wakati 

Kamati hiyo ilipokutana na Kamati ya Bunge ya 

Utawala na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma. Kulia

 kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Laurean 

Ndumbaro.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala 

na Serikali za Mitaa akifuatilia majadiliano ya 

Wajumbe 

wa Kamati yake wakati Kamati hiyo ilipokutana na 

Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa 

Umma na Utawala kwa ajili ya kupokea na kujadili 

Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa Utumishi na 

Mshahara Serikalini (MCMIS), Kulia kwake ni Katibu wa 

Kamati hiyo, Eunike Shirima.

No comments:

Post a Comment