WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 26, 2018

KAMATI YA PAC YATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA VETA MWANZA NA MRADI WA UJENZI WA ROCKY CITY MALL

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu John Mongela wakitoka ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kuanza  ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Jiji hilo.

 Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakionyeshwa baadhi ya vifaa  vilivyonunuliwa kwa  ajili ya Karakana inayoendekea kujengwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akiongozana na uongozi wa Mamlaka ya Ufundi Stadi  VETA kwenda kukagua mradi wa ujenzi wa Karakana unaotekelezwa na Mamlaka hiyo

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakielekea kukagua Mradi ya ujenzi wa Karakana unaotekelezwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mwanza baada ya Kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa Karakana.

Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)  wakiwasili katika Jengo la Rocky City Mall lililopo Jijini Mwanza kwa ajili ya kukagua mradi huo uliotekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Mfuko wa Pensheni wa LAPF. Mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Ndugu Eliudi Sanga.

Wajumbe wa Kamati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakionyeshwa baadhi ya maeneo ndani ya Jengo la Rocky City Mall. Pichani wakiangalia chumba ambacho kinadhibiti hali ya usalama katika maeneo yote ya jengo hilo


Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)  wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kujadili utekelezaji wa mradi wa Jengo la  Rocky City Mall  unaotekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji hilo na LAPF. 


No comments:

Post a Comment