WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, March 20, 2018

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA LAAC NA PAC ZAPATIWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), baada ya wajumbe hao kupatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi. Semina hiyo imefanyika katika Ofisi za Ukaguzi Mkoa wa Iringa.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakifuatilia mada katika semina iliyohusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika Mkutano wa Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment