WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, May 30, 2018

SPIKA NDUGAI AFIKA KUWASABAI WAFIWA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KATIKA MSIBA WA MAREHEMU KASUKU BILAGO.

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waombolezaji nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu alipofika kuwasabia wafiwa na kuaga mwili wa marehemu Mjini Kakonko, Mkoani Kigoma
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu alipofika kuwasabia wafiwa nyumbani kwa Marehemu Mjini Kakonko, Mkoani Kigoma
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiwasabai watoto wa marahemu, Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto)akimfariji Mke wa marehemu Bi. Pietha Bisangwa Bilago leo Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia) nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, marehemu Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai  (katikati) akiteta jambo na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe (kulia) na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, marehemu Kasuku Bilago Wilayani kakonko Mkoani Kigoma.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu katika msiba huo
Mbunge wa Kasulu  Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Kigoma Mhe. Daniel Nsanzugwako akizungumza katika msiba huo. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbozi Mhe. Pascal Haonga ambaye alikuwa rafiki wa karibu na marehemu wakati akiwa Katibu wa Chama cha Walimu Wilayani Mbozi.

Tuesday, May 29, 2018

NAIBU SPIKA AONGOZA WAHESHIMIWA WA BUNGE KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUNGU MAREHEMU KASUKU BILAGO

 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza  wakati wa tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiweka shada la maua  wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago. Mara baada ya tukio hilo mwili huo ulisafirishwa kwenda Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson  (wa pili kulia) akizungumza na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (wa pili kushoto), Mbunge wa Vunjo, Mhe. James Mbatia (kushoto) na Mbunge wa Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya (kulia) wakati wakusafirisha mwili wa aliyekuwa  Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Bilago katika Uwanja wa Ndege wa Jijini Dodoma

MAJONZI BUNGENI



 Naibu Spika  wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuletwa Bungeni kesho Jumanne tarehe 29 Mei, 2018 kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Kasuga, Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma. Awali mapema leo, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo.



Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.



Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago


Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt. George akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.



Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mhe. Salma Kikwete  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.



Mbunge wa Tarime Mjini , Mhe. Esther Matiko akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.


Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Aliyeketi kusaini ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mhe. Mahmoud Mgimwa

Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.