WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, June 13, 2018

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI CHA KUPOKEA TAARIFA YA MAJUMUISHO KATI YA KAMATI YA BAJETI NA SERIKALI

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya Kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto kwa Spika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya Kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto kwa Spika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia (wa pili kulia) akizungumza na Mawaziri, Wenyeviti wa Kamati za Bunge na Watendaji Wakuu Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katikati  ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu

WANAFUNZI WATEMBELEA BUNGE KWA LENGO LA KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mount Kibo ya Jijini Dar es salaam wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa

Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Angelico Lipani ya Jijini Arusha wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.


Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Martin Luther ya Jijini Dodoma wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.

Monday, June 11, 2018

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA WADHAMINI YA CHUO KIKUU CHA DODOMA


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Bodi ya wadhamini ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Ami Mpungwe (wa tatu kushoto)


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akifafanua jambo mbele ya Wajumbe kutoka Bodi ya wadhamini ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Ami Mpungwe (wa tatu kushoto)