WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Saturday, June 2, 2018

KAMATI MAALUM ZA BUNGE ZA KIUCHUNGUZI KUHUSU SEKTA ZA UVUVI WA BAHARI KUU NA GESI ASILIA ZAWASILISHA TAARIFA ZAKE NA MHE. SPIKA KUZIPOKEA NA KUZIKABIDHI SERIKALINI

    Spika wa Bunge (Mb), Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla ya uwasilishwaji na kukabidhi taarifa za Kamati Maalum alizounda  kuchunguza na kushauri kuhusu sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi asilia. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na mara baada ya kuzipokea taarifa hizo Mhe. Spika alizikabidhi Serikalini ambapo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.

 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Gesi Asilia Mhe. Dustan Kitandula (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipokea taarifa za Kamati Maalum za Bunge kwa niaba ya Waziri Mkuu zilizoundwa kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia kutoka kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Wengine katika picha kutoka kushoto kwa Mhe. Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.

   Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kamati Maalum ya Bunge aliyounda kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Gesi Asilia (waliosimama) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kutoka kushoto kwa waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwepo niaba ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dustan Kitandula, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi.
pika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kamati Maalum ya Bunge aliyounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu (waliosimama) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi.

Na Debora Sanja-Bunge
Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), amepokea na kukabidhi Serikalini Taarifa za Kamati Maalum alizounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia.

Taarifa hizo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Juni 2, mwaka 2018 na kuhudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge na viongozi mbalimbali wa
Kitaifa.


Taarifa ya Kamati Maalum ya Sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu iliwasilisha
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura na kwa upande wa Kamati
Maalum ya Nishati ya Gesi aliwasilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.
Dunstan Kitandula.

Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa taaarifa za Kamati hizo,
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai alisema kuundwa kwa Kamati hizo ni
kutimiza wajibu wa Wabunge kuisimamia na kuishauri Serikali hasa
katika maeneno ambayo bado hayana mchango wa kutosha katika
kuinufaisha nchi.

“Nawashukuru wajumbe wa Kamati zote mbili kwa kazi nzuri iliyotukuka,
tatizo kubwa tumeona lipo katika mikataba, inatuumiza sana,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mhe.
Profesa Makame Mbarawa alimshukuru Mhe. Spika kwa uzalendo wake kwa
kuwa bila yeye ripoti hizo zisingekuwepo.

Aliwashukuru pia Wenyeviti wa Kamati zote mbili na wajumbe wake kwa
kufanya kazi kwa uzalendo usiku na mchana na kutoa ripoti zilizosheheni
mapendekezo ambayo yakifanyiwa kazi nchi itasonga mbele.

“Tutasoma kila kitu katika ripoti hizo na kuwahakikishia kwamba
mapendekezo yote yatatekelezwa kwa ukamilifu ndani ya muda mfupi,
wahusika wote waliotajwa kwa tuhuma mbalimbali kwenye ripoti, uchunguzi
utafanyika na sheria itachukua mkodo wake,” alisema.

Mhe. Spika aliunda kamati hizo Novemba 17 kwa lengo la kuchunguza na
kushauri sababu za sekta hiyo kutochangia ipasavyo katika Pato la
Taifa.


No comments:

Post a Comment