WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 29, 2018

KAMATI YA MADINI YAENDELEA NA VIKAO JIJINI DODOMA

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo imekutana na Wizara ya Madini kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini Ndugu Augustine Ollal akiwasilisha taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 katika kikao cha Kamati ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Oofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wengine ni manaibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo (katikakati) na Mhe. Doto Biteko.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati  na Madini Mhe. Mariam Ditopile akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa  Wizara ya Madini  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendelepkatika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Felister Mgonja.


No comments:

Post a Comment