KAMATI YA SHERIA NDOGO YAKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA FEDHA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt
Ashatu Kijaji na Kaimu Mkurugenzi wa
Masuala ya Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipanfo Ndg. Elias Kalist wakiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Sheria Ndogo walipopeleka majibu ya Serikali yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria
Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge la Kumi na Moja
leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Sheria Ndogo Mheshimiwa William Ngeleja akisisitiza jambo wakati Kamati yake
ilipokutana na Wizara ya Fedha na Mipango kupokea na kujadili majibu ya Serikali yatokanayo
na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili
wa Bunge la Kumi na Moja leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria
Ndogo wakiendelea na majadiliano wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara ya
Fedha na Mipango kupokea na kujadili majibu ya Serikali yatokanayo na Uchambuzi
wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge la
Kumi na Moja leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment