SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BUNGE LA CHINA
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Mgeni wake Mheshimiwa Prof. Lou
Jiwei ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China
(CPPCC) alipomtembelea hii leo na kufanya nae mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika
Jijini Dodoma.
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimvalisha vazi la Kimasai mgeni wake ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa
Prof. Lou Jiwei kama ishara ya Utamaduni wa Kitanzania walipokutana na kufanya
mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma hii leo.
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa
Wang Ke alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo hii leo kwenye Ukumbi wa Spika
Jijini Dodoma. Balozi huyo aliambatana na ujumbe kutoka Bunge la China ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya
Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou
Jiwei.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Wageni
kutoka China wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya
Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei (kulia kwa Spika) walipokutana hii leo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma,
kushoto kwa Spika ni Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Wang Ke. Baadhi ni Watumishi wa Ofisi ya Bunge.
Wageni
wa Mheshimiwa Spika kutoka nchini China wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei wakipewa
maelekezo kuhusiana na mpangilio wa ukaaji Bungeni kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa – Ofisi ya Bunge, Ndg.
Daniel Eliufoo walipotembelea Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
No comments:
Post a Comment