WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, November 27, 2018

BUNGE SPORTS CLUB YAAHIDI USHINDI MICHUANO YA EALA

Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge "Ndugai Boys", William Ngeleja akiambaa na mpira wa kati wa mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Mabunge ya Jumuia ya Afrika Mashariki jijini Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Ngela pia ni Mwenyekiti wa Bunge Sports Club.


Naibu Waziriu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na mchezaji wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge , Dk. Angelina Mabula akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Chuo cha Mipango wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu . Bunge Queens inajiandaa na michezo ya Mabunge ya Jumuia ya Afrika Mashariki itakayofanyika Bujumbura Burundi kuanzia Desemba mosi mwaka huu 

Wachezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanaume) Mhe. Aeshi Hillary Mhe. Seif Gulamali na Mhe. David Silinde wakifanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao.



Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Rita Kabati akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mhe. Faida Bakari.


Mchezaji wa mpira wa Wavu wa Bunge, (Wanawake) Mhe. Neema Mgaya akipiga mpira wakati wa mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Kushoto ni Mheshimiwa Rita Kabati.


Wachezaji wa Bunge Sports Club, kutoka kushotoFlatei Massay, Venance Mwamoto na Angelina Mabula wakifanya mazoezi Uwanja wa Jamhuri

No comments:

Post a Comment