WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, January 16, 2019

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAENDELEA NA VIKAO BUNGENI JIJINI DODOMA

Mshauri wa mambo ya sheria Ofisi ya Bunge, Ndugu SerafineTamba akizungumza katika kikao cha Kamati ya Miundombinu kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo alikuwa akiwapitisha wajumbe wa Kamati hiyo katika Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini wa mwaka 2018.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Kakoso akifafanua jambo katika kikao cha kamati  hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma , katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Ndugu Giliard Ngewe

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Ndugu Giliard Ngewe akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini, 2018 katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mindombinu kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Ndugu Giliard Ngewe katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe akifuatiia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Miundmbinu kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo amewasili maelezo ya Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa mwaka 2018 mbele ya Kamati hiyo.kushoto  Naibu Waziri, Mhe. Atashasta Nditiye.

No comments:

Post a Comment