WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Sunday, January 20, 2019

WAJUMBE WA KAMATI TATU ZA BUNGE WAJENGEWA UELEWA KUHUSU MISWADA MIWILI ILIYOSOMWA BUNGENI

Wajumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kujengewa uelewa kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa mwaka 2018 na Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018.kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Ndugu Gilliard Ngewe katika kikao cha pamoja cha kamati hizo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Ndugu Gilliard Ngewe akitoa mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018 kwa wajumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika kwenye kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ndugu Mussa Zungu.


Mwezeshaji kutoka Wizara ya Maji, Ndugu Simon Nkanyemka akitoa mada kuhusu Sheria na Mifumo katika Usimamizi na Uendeshaji wa Sekta ya Maji kwa wajumbe wa  Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

No comments:

Post a Comment