Mpambe wa Rais akiingia
Bungeni kuwasilisha bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Mhe. Rais
kwa ajili ya kudhibitishwa na Bunge.
Spika wa Bunge, Mhe. Job
Y. Ndugai akionesha kwa Waheshimiwa Wabunge bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu
mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mpambe wa Rais.
Spika wa Bunge, Mhe. Job
Y. Ndugai (kulia) na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai (katikati) wakifungua
bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu kutoka kwa Mheshimiwa Rais. Kushoto ni Mpambe
wa Rais.
Spika wa Bunge, Mhe. Job
Y. Ndugai (kulia) akitangaza Jina la
Waziri Mkuu mara baada ya kupokea bahasha yenye jina hilo kutoka kwa Mhe. Rais.
Mbunge wa Ruangwa, Mhe.
Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Ruangwa, Mhe.
Kassim Majaliwa akizungumza mara baada ya kudhibitishwa na Wabunge kuwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bunge limemthibitisha Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi,
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano mingine
(2020-2025) kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge sawa na asilimia
100.
Akitangaza matokeo ya kura, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema
katika ya kura zote 350 zilizopigwa hakukuwa na kura ya hapana wala kura
iliyoharibika.
“Kura zote zilizopigwa ni 350 hakuna iliyoharibika, hakuna kura
ya hapana. Kura zote 350 zimemthibitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,
kwa hiyo ndugu wabunge Mheshimiwa Majaliwa amethibitishwa na Bunge hili kuwa
Waziri Mkuu kwa kura 350 sawa na asilimia 100.
Awali jina la Waziri Mkuu mteule liliwasilishwa Bungeni na
Mpambe wa Rais na kukabidhiwa kwa Mheshimiwa Spika.
Akizungumza
baada ya kuthibitishwa Mheshimiwa Majaliwa amesema amepokea uteuzi huo kwa
mikono miwili na anamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kuwapa uhai wote
na kushuhudia hayo, Pia amemshukuru Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kwa imani kubwa aliyoionesha juu yake.
“Mheshimiwa Spika jambo hili si dogo, Mwenyezi Mungu
ameliongoza, namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa imani kubwa
aliyonayo juu yangu na kuendelea kuniamini. Namshukuru sana na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ushiriki wake katika kuridhia jina langu.”
Alisema.
Mheshimiwa Majaliwa alimpongeza pia Mheshimiwa Spika kwa
kuchaguliwa bila kupingwa kuwa mbunge wa Kongwa pamoja na kurudi katika nafasi
yake ya uspika baada ya kupigiwa kura nyingi na waheshimiwa wabunge.
Awali kabla ya kuthibitisha jina la Waziri Mkuu wabunge
mbalimbali walizungumzia utendaji kazi wa Mheshimwa Majaliwa ambapo Mbunge wa
Tunduma, Mheshimiwa David Silinde alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa kumrudisha tena Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika nafasi
hiyo.
Wabunge wengine waliopata fursa ya kumpongeza na kuzungumzia
utendaji wake ni pamoja na Mheshimiwa William Lukuvi, Mheshimiwa Kapten Mstaafu
George Mkuchika, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mheshimiwa Fakharia Shomari na
Mheshimiwa Januari Makamba.
No comments:
Post a Comment