Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12, Bungeni Dodoma.
Bunge limechagua Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Spika wa
Bunge la 12.
Akitangaza matokeo hayo mara baada ya uchaguzi kufanyika, Spika wa
Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema Dkt. Tulia amepata kura 350 kati ya kura
354 zilizopigwa.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, aliwashukuru Wabunge
wote kwa ushindi huo wa kishindo na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega bila
kujali tofauti za kisiasa.
“Naahadi nitawatumikia, nitafanya kazi kwa ufanisi katika kazi
zangu kama Naibu Spika, msisite kuniletea hoja zenu pale mnapukuwa nazo,”
alisema
Aidha,
alisema atamshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumkia uzoefu
alionao ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.
No comments:
Post a Comment