Wachezaji wakishangilia baada ya kubeba vikombe
Naibu Spika na Timu ya Netibali wakichukua kombe lao
Wachezaji wa Mpira wa Kikapu wakibeba Kombe lao
Wachezaji wa Mpira wa Wavu wakibeba Kombe lao
Mhe. Simai akivishwa medali baada ya kuibuka mshindi wa pili mchezo wa kutembea kwa kasi
Naibu Spika akifurahia medali yake baada ya kuibuka mshindi wa pili mchezo wa kutembea kwa kasi kwa upande wa Wanawake
Mashindano ya 11 ya Mabunge Wanachama
wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki yaliyokuwa yakifanyika Jijini Arusha yamemalizika huku
Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikishinda vikombe
nane.Timu zilizoibuka washindi wa jumla na kuwa Mabigwa ni pamoja
na;
·
Timu ya Mpira wa Miguu
· Timu ya Mpira wa Pete (Netball)
· Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanaume
· Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) Wanawake
· Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball)
Wanaume
· Timu ya Mpira wa Kikapu ( Basketball)
Wawake
· Timu ya Kuvuta Kamba Wanaume
· Timu ya Riadha Wanawake
Aidha
katika mashindano mingine Timu za Bunge la Tanzania zimeibuka Washindi wa Pili
katika michezo ifuatayo;
· Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanawake-Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson
aliibuka Mshindi wa Pili.
· Mchezo wa Kutembea kwa kasi Wanaume-Mbunge wa Nungwi, Mhe. Simai Hassan Sadik
aliibuka Mshindi wa Pili
· Timu ya Kuvuta Kamba Wanawake waliibuka Washindi wa Pili
· Mchezo wa Darts Timu ya Wanaume wallibuka Washindi wa Pili.
Michezo
ya Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilihusisha Timu kutoka
Mabunge 6 ya Tanzania, Kenya, Burundi, Zanzibar, Sudan Kusini, Uganda na Bunge
la Afrika Mashariki ambao walikuwa wenyeji.