WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, February 24, 2022

SPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI SEMINA YA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI, MAKAMU WENYEVITI WA KAMATI NA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge katika semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao wa Wabunge yanayoendelea katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, Februari 24, 2022, kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu (Mb)



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu (Mb), akiongoza semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea leo katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, Februari 24, 2022, kushoto ni Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb)



Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Ndg. Kadari Singo akiwasilisha mada kuhusu misingi ya uongozi na utawala bora wakati wa semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, Februari 24, 2022



Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge wakiwa katika semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao wa Bunge yanayoendelea katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, Februari 24, 2022, kuanzia kushoto ni Wabunge wa Viti Maalum, Mhe. Halima Mdee, Mhe. Alice Kaijage na Mhe. Fatma Toufiq 



Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo (Mb), akichangia mada wakati wa majadiliano katika semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa kamati ya uongozi, Makamu Wenyeviti wa kamati na Tume ya Utumishi wa Bunge yanayoendelea katika ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar, Februari 24, 2022, kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliazer Feleshi, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Madaba, Mhe. Joseph Mhagama (kushoto)


 

No comments:

Post a Comment