WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, February 28, 2022

SPIKA DKT. TULIA NA MBUNGE WA MBEYA MJINI ATOA MCHANGO WA MIFUKO 200 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI ITEZI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akikabidhi mifuko 200 ya saruji kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Itezi, Ndg. Betseba Nsemwa ikiwa ni mchango wake kwa Shule hiyo tukio lililofanyika leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022, Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dormohamed Rahmat na kulia ni Diwani wa kata ya Itezi, Mhe. Sambee Shitambala wengine ni Vijana kutoka Taasisi ya Tulia Trust


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itezi wakati alipowasili Shuleni hapo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022, kulia mbele ni Diwani wa kata ya Itezi, Mhe. Sambee Shitambala


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itezi (hawapo kwenye picha) wakati alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022, kushoto ni Mbunge wa Mchinga, Mhe. Salma Kikwete na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dormohamed Rahmat


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itezi wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza wakati alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022


Wananchi Mbalimbali wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Itezi wakati alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022



 

No comments:

Post a Comment