WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, March 23, 2022

KAMATI YA LAAC YA KAGUA MRADI WA STENDI HALMASHAURI YA ILEMELA






LAAC yaipongeza Ilemela Ukamalishaji wa Mradi wa Stendi


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Serikali za mitaa(LAAC) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza kwa ukamilishaji wa mradi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori.

Hayo yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Zedi (Mb) wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo.

‘’ Kamati yetu imeridhika kabisa na matumizi ya pesa ya mradi huu pia  nakipongeza chuo kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM) kwa kuweza kuchora mchoro wa mradi huu wa stendi ’’ alisema Mhe. Zedi.

Mhe.Zedi aliupongeza uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kukamilisha mradi huo pamoja na kusaidia utumiaji mzuri wa fedha za mradi

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Robert Gabriel alisema watafanyia kazi mapendekezo ya Kamati pamoja na maagizo yote waliopewa na kamati. Alisema Halamashauri ya Manispaa ya Ilemela inafanya vyema katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment