WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, March 22, 2022

KAMATI YA LAAC YAKAGUA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI WILAYA YA MAGU

 





                                                           

    Na. Zanele Chiza

KAMATI YA LAAC YAKAGUA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU.

Kamati ya Bunge ya LAAC imekagua ujenzi wa ofisi ya Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi, Kaimu Mwenyekiti Mhe. Aloyce Kwezi (Mb) ameipongeza Halmashauri kwa jengo imara litalowafikishia huduma wananchi kwa ukatibu.

Pia, amewataka TAMISEMI kuhakikisha inaleta fedha zilizobaki ili kuweza kukamilisha mradi uliochukua zaidi ya miaka kumi.

Wakati huo huo, Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewahakikishia kamati kuwa amepokea maelekezo ya kuleta fedha kwa mradi huo uliogharimu takribani bil 7 na utaisha kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Ngusa Samike amepokea salamu za pongezi na kusema ushirikiano wa viongozi wa Mkoa umeweza kuleta mafanikio. Kukosekana kwa migogoro ndio kumeleta mafanikio Halmashauri ya Magu.



No comments:

Post a Comment