Matukio katika picha yaliyojiri wakati Spika wa Bunge, Mhe.
Dkt. Tulia Ackson akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.
No comments:
Post a Comment