Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akichangia mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika wakati wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022.
Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.
Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) kutoka Bunge la Tanzania wakishiriki katika Mkutano wa 51 wa SADC – PF wenye mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022. Kuanzia kushoto ni Mhe. Shally Raymond, Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim
No comments:
Post a Comment