Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Spika wa Bunge la Korea Kusini,
Mhe. Jin Pyo Kim katika ofisi ndogo za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145
wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.
Mhe. Spika ameambatana na Wabunge wa Bunge
la Tanzania ambao ni Wawakilishi katika Umoja huo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge
Spika wa Bunge la Korea Kusini, Mhe. Jin Pyo Kim tukio lililofanyika katika ofisi
ndogo za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe
12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)
unaoendelea nchini humo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiagana na Spika wa Bunge la Korea Kusini,
Mhe. Jin Pyo Kim baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba,
2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea
nchini humo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.
No comments:
Post a Comment