WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, July 27, 2023

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE LA ITALIA.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Italia, Mhe. Lorenzo Fontana alipomtembelea leo tarehe 27 Julai, 2023 ofisini kwake Jijini Roma nchini Italia.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimpatia zawadi ya ngao yenye nembo ya Bunge la Tanzania Spika wa Bunge la Italia, Mhe. Lorenzo Fontana alipomtembelea leo tarehe 27 Julai, 2023 ofisini kwake Jijini Roma nchini Italia.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiambatana na Spika wa Bunge la Italia, Mhe. Lorenzo Fontana alipomtembelea leo tarehe 27 Julai, 2023 ofisini kwake Jijini Roma nchini Italia.

Tuesday, July 25, 2023

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma nchini Italia tarehe 24 Julai, 2023.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia tarehe 24 Julai, 2023, aliesimama ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alipomtembelea tarehe 24 Julai, 2023 katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma nchini Italia. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (watatu kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (watano kushoto) alipomtembelea tarehe 24 Julai, 2023 katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma nchini Italia. Wapili kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc, pamoja na Maafisa kutoka Ofisi ya Bunge na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.


 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma nchini Italia tarehe 24 Julai, 2023.

Monday, July 3, 2023

RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 53 WA SADC PF JIJINI ARUSHA


Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha na kupokelewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc



Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakielekea ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha.



Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC uliofanyika leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha na kufunguliwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Katibu wa Bunge la Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza wakati wa Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC uliofanyika leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha na kufunguliwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Kwaya ya Bunge ikiimba wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha, uzinduzi huo umefanywa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha.

 

Wabunge wa Bunge la Tanzania wakishiriki katika uzinduzi wa Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha, uzinduzi huo umefanywa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan 


Wajumbe wa Jukwaa la SADC wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufungua Mkutano wa 53 wa Jukwaa hilo leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha. Watatu kushoto waliokaa ni mwenyeji Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Rais wa SADC PF na Spika wa Bunge la Seychelles, Mhe. Roger Mancienne (Watatu kulia waliokaa).



Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson mara baada ya kufungua Mkutano wa 53 wa Jukwaa la SADC leo tarehe 3 Julai, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha.