WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, August 18, 2023

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA NISHATI




Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili mbele ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Iddi Kassim Iddi akijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.



Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato

Mwenyekiti wa Bodi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ndg. Janeth Mbene akitolea maelezo hoja za Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia ni Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Iddi Kassim Iddi.


 

No comments:

Post a Comment