Tuesday, October 31, 2023
MKUTANO WA KUMI NA TATU WA BUNGE WAANZA JIJINI DODOMA
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimuapisha Mbunge wa Mbarali Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Mbunge wa Mbarali Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo akila kiapo cha Uaminifu
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Waheshimiwa Wabunge wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge umeanza Jijini Dodoma ambapo shughuli ya kwanza katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano Mkutano huo ilikuwa ni Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) kumuapisha Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo ambaye alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Marehemu Francis Mtega.
Aidha, katika Mkutano huu Bunge
linatarajia kujadili na kupitisha Maazimio yafuatayo;
Azimio la
Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Tulia Ackson Mb, kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Azimio la
Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya
Afrika la Mwaka 2023 (Treaty for Establishment of the African Medicines Agency
– AMA).
Azimio la
Bunge kuhusu Mapendekezo ya Tanzania Kuridhia Kujiunga na Mkataba wa Wakala wa
Kimataifa wa Nishati Jadidifu la Mwaka 2009 (Statute of the International
Renewable Energy Agency – IRENA).
Kwa upande mwingine katika Mkutano huu Bunge linatarajia kujadili
Miswada ifuatayo;
Muswada wa
Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2023 [The Written
Laws (Miscellaneous Amendments) (No.4) Bill, 2023] .
Muswada wa
Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Sekta ya Sheria wa Mwaka 2023
[The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023].
Muswada wa
Sheria ya Bima ya Afya kwa wote wa Mwaka 2023
Mbali na hayo katika Mkutano huu
Bunge linatarajia kupokea na kujadili taarifa za Kamati za PAC na LAAC kuhusu
Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Taarifa ya Kamati
ya PIC kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
Katika Mkutano huu Bunge pia
linatarajia kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha
2024/2025.
Monday, October 30, 2023
WAZIRI MKUU AWAONGOZA VIONGOZI, WABUNGE, WATUMISHI WABUNGE NA WANANCHI MBALIMBALI KATIKA KUMPOKEA RAIS WA IPU JIJINI DODOMA
RAIS WA IPU AWAOMBA WATANZANIA USHRIKIANO ILI KUONESHA UTOFAUTI
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson ameomba ushirikiano kutoka kwa Watanzania wote ili kuionyesha Dunia utofauti wa Tanzania kuishika nafasi hiyo.Waziri
Mkuu
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.
Mheshimiwa Oran Njeza
------------------------------------
Friday, October 20, 2023
Thursday, October 19, 2023
WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU WAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA UJENZI KUHUSU UTENDAJI WA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA).
Wajumbe wa kamati
ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Mhe. Selemani Kakoso wamepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Ujenzi kuhusu
utendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha Julai - Oktoba,
2023; Mafanikio na Changamoto katika kikao kilichofanyika leo tarehe 19 Oktoba,
2023 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Aidha, kikao hicho
kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro.