WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 18, 2024

KAMATI YA PAC YAKAGUA MRADI WA KUTOA MAJI ZIWA VIKTORIA NA KUSAMBAZA KATIKA MIJI YA TABOTA, IGUNGA NA NZEGA






















 

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kupokea maji kutoka Ziwa Viktoria na kusambaza katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega uliotekelezwa na Wizara ya Maji.

 

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb) wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo na baadae kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya Kwanza na ya pili.

 

Alisema Kamati inaipongeza TUWASA kwa kusimamia vizuri mradi huo na kufikia malengo ya Serikali ya kufikisha maji safi na salama kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa ukame ambayo hayana vyanzo vya maji vya uhakika.

 

“TUWASA mmejitahidi sana, kwa macho tumejionea ubora wa miundombinu, sasa katika uendelevu wa mradi mlioueleza jitahidini na maeneo yaliyobakia ya Sikonge, Urambo Isikizya, kaliua, Shelui na Tinde maji yawafikie wananchi.” Alisema

 

Mheshimiwa Hasunga aliwasisitiza TUWASA kuhakikisha wanaongeza umakini na usimamizi wa miundombinu ya mradi huo kwa lengo la kuondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huo.

 

“Kwenye changamoto ya upotevu wa maji tutaendelea kupambana, ongezeni usimamizi ili maji yasipotee yawafikie wananchi.” Alisema

 

Mapema akiwasilisha taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Tabora (TUWASA) Mhandisi Mayunga Kashilimu amesema kukamilika kwa mradi huo kumewezesha wananchi zaidi ya milioni moja na laki mbili (1,200,000) wanapata huduma ya maji safi na salama.

 

“upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka hadi kufikia asilimia 100 katika Manispaa ya Tabora na miji ya Igunga, Nzega, Makao makuu ya Wilaya ya uyui pamoja na vijiji 102

 

Alisema  huduma bora ya Maji inachangia kuboresha afya za wananchi wa maeneo husika na kuinua uchumi kupitia maendeleo ya sekta zingine zinazotegemea maji kama vile viwanda.

 

Kamati ya PAC, kesho inatarajia kukagua mradi wa kiwanda cha kupaka rangi mabomba kwa ajili ya kuweka mfumo wa upashaji joto mabomba katika  mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga

 

 Mwisho

No comments:

Post a Comment