WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, October 18, 2016

KAMATI YA LAAC YAKATAA TAARIFA YA HESABU YA HALMSHAURI YA JIJI LA MBEYA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Abdalla Chikota akisisitiza jambo katika Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Dodoma. Katika kikao hicho wajumbe wa Kamati ya LAAC waliiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenda kuiandaa upya taairfa yao hesabu kutokana na kubaini kuwapo kwa mapungufu.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)  wakiendelea na kikao chao leo Mjini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa wakijadili masuala mbalimbali katika kikao cha Kamati kilichofanyika leo Mjini Dodoma. Kamati hiyo ilikuwa inafanya mahojiano na Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuhusu hesabu za mwaka wa fedha 2014/2015

Monday, October 17, 2016

VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE VYAANZA LEO MJINI DODOMA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa Josephat Kandege akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) leo Mjini Dodoma .

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Juma Hamad Omar akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Bajeti kilichofanyika leo Mjini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakijadili jambo mara baada ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyochukuliwa na Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka, Uchaguzi huo umefanyika leo Mjini Dodoma

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akisikiliza maoni ya wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao cha Kamati kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Aeshi Hilary akichangia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Thursday, October 13, 2016

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA UKIMWI YACHAGUA VIONGOZI

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi uliofanyika  Mjini Dodoma, kushoto ni Makamu Mwenyekiti mpya wa Kamati hiyo, Dkt. Jasmine Tisekwa

Wajumbe wapya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, Uchaguzi huo ulifanyika katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.

Wajumbe wapya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI wakiendelea na kikao cha uchaguzi katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, Katika uchaguzi huo Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku Dk. Jasmine Tisekwa akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Wednesday, October 5, 2016

SPIKA WA BUNGE MHESHIMIWA JOB NDUGAI APOKEA UJUMBE WA BARUA KUTOKA KWA SPIKA WA BUNGE LA PAKSTANI MHESHIMIWA SARDAR AYAZ SADIQ.


1.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Pakstani Nchini Tanzania Mheshimiwa Amir Mohamed Khan wakati Balozi huyo alipomtembelea Ofini kwake leo Mjini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akipokea barua kutoka kwa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Pakistani Mheshimiwa, Sardar  Ayaz Sadiq iliyowasilishwaa leo ofisini kwake Mjini Dodoma na Balozi wa Pakstani Nchini Tanzania Mheshimiwa Amir Mohamed Khan.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimsikiliza Balozi wa Pakstani nchini Tanzania Mheshimiwa Amir Mohamed Khan.
mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Pakistani Mheshimiwa, Sardar  Ayaz Sadiq, tukio hilo limefanyika leo Ofisini kwa Mheshimiwa Spika Mjini Dodoma.