WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, March 21, 2018

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA LAAC NA PAC WAENDELEA NA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KATIKA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI MKOANI SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  ukaguzi wa ufanisi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Jmaes Pilly katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  ukaguzi wa ufanisi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Jmaes Pilly katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad.

 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa  Mussa Assad akisisitiza jambo katika semina kwa  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Mkoani Singida ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Tuesday, March 20, 2018

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA LAAC NA PAC ZAPATIWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), baada ya wajumbe hao kupatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi. Semina hiyo imefanyika katika Ofisi za Ukaguzi Mkoa wa Iringa.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakifuatilia mada katika semina iliyohusu masuala mbalimbali yanayohusu ukaguzi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika Mkutano wa Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoani Singida.

Monday, March 19, 2018

KAMATI YA LAAC NA PAC ZAANZA ZIARA MKOA WA SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wameanza ziara ya siku tano Mkoa wa Singida, pichani wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Rehema Nchimbi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu  za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hizo zilipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuendelea na ziara Mkoani humo.  

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu  za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kamati hizo kukagua Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Singida